Entertainment

RAPA JULIANI ATAJWA KUSHIRIKI MPANGO WA EISENHOWER FELLOWSHIP

RAPA JULIANI ATAJWA KUSHIRIKI MPANGO WA EISENHOWER FELLOWSHIP

Rapa Juliani amechaguliwa kujiunga na mpango wa Eisenhower Fellowships ambayo inatarajiwa kuanza Aprili 10 hadi mei 18 mwaka wa 2023.

Juliani ameweka wazi taarifa hiyo kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram kwa kusema kuwa amefarijika kuwa miongoni mwa viongozi wa afrika ambao watasafiri nchini marekani kwa ajili mpango huo ambao umefadhiliwa kwa asilimia kuhudumia mahitaji ya washirika wake.

Ushirika wa Eisenhower Fellowships ulibuni mwaka wa 1953 kwa ajili ya kutoa heshima kwa rais Dwight D. Eisenhower kwa mchango wake mkubwa wa kupigania haki za kibinadamu kama kiongozi wa dunia.

Utakumbuka Juliani amechagulia kujiunga na ushirika huo kupitia wakfu wake wa Dandora hiphop city na atapata fursa ya kusafiri marekani kwa wiki 4 hadi 6 kupata elimu lakini pia kubadilishana mawazo na watu mbali mbali duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *