
Msanii wa muziki kutoka 001 music Happy C ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Beyond Infinity.
Beyond Infinity EP ina jumla ya ngoma 5 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Chikuzee na K.O.
EP hiyo ina nyimbo kama Yatakwisha, Inakera, Maupendo, Coco, na Heshima.
Beyond Infinity inaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima happy c ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2021 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo Karata 3 ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju tatu ya moto.