
Msanii wa Bongofleva Harmonize amemvisha pete ya uchumba Mwigizaji Kajala Masanja ikiwa ni siku chache toka wawili hao warudiane baada ya penzi lao kuvunjika kipindi cha nyuma.
Tukio hilo limefanyika Jumamosi Juni 25,mwaka 2022 katika hoteli ya Serena huku likihudhuriwa na watu wa karibu wa wasanii hao ukiwemo uongozi wa lebo ya Konde Gang.
Wakati wa tukio hili Harmonize amekiri kwamba Kajala ni Mwanamke bora kwake na kuna wakati Kajala alimpa hifadhi kwenye nyumba yake wakati Harmonize akiwa hana nyumba.
Harmonize na Kajala wamechumbiana ikiwa ni takribani mwaka mmoja tangu walipotengana baada ya mwanamuziki huyo kumfungulia mashtaka Kajala na binti yake Paula akiwatuhumu kuvujisha picha zake za utupu