Entertainment

KING SAHA AMJIBU KISOMI ALLAN HENDRICK

KING SAHA AMJIBU KISOMI ALLAN HENDRICK

Mwanamuziki kutoka Uganda King Saha amethibitisha kuwa hawezi mujibu kijana wa Bebe Cool Allan Hendrick ambaye alimshambulia kupitia wimbo uitwao Matayo ambao aliuachia jumatatu wiki iliyopita.

Katika mahojiano yake hivi karibuni King Saha ameeleza adui yake ni Bebe Cool na sio mwanae Allan Hendrick. Msanii huyo amesema Allan Hendrick anatumia jina lake kutafuta umaarufu.

“Sitamjibu Hendrick kwa kuwa sijui nia yake. Labda anataka wamzungumzie kwenye vyombo vya habari ila nina shida na Zakayo ambaye Baba yake mzazi”,Alijibu alipoulizwa atoe maoni kuhusu wimbo wa Matayo wake Allan Hendrick.

Hata hivyo Hendrick amesisitiza kuwa wimbo wa Matayo ni mahususi kwa ajili ya King Saha na kila kijana ambaye ameathirika na matumizi ya dawa za kulevya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *