
Msanii wa muziki wa dancehall kutoka nchini uganda Karole Kasita amefunguka na kudai kwamba hataki kabisa kufunga ndoa kwa njia ya harusi.
Karole kasita amesema hana imani tena na wanaume na hivyo haoni akimtambulisha mwanaume yeyote kwa wazazi wake hivi karibuni.
Hitmaker huyo wa Balance amesema anafadhalisha mahusiano yake yawe ya siri kwani kuna aibu kubwa uibuka wakati mwanamke anapoachwa baada ya harusi.
Kauli yake imekuja mara baada ya kuumizwa kwenye mahusiano yake ya zamani baada ya kuachwa na mchumba kipindi yupo chuo kikuu, hivyo hanawaogopa wanaume wote kwani wanaweza kumkimbia.
|