
Mwanamuziki kutoka Uganda Eddy Yawe amekiri kuchoshwa na kitendo cha kuwa mstari wa mbele kutatua tofauti za Bobi Wine na wasanii wenzake kila mara wanapoingia kwenye ugomvi.
Katika mahojiano yake hivi karibuni Eddy Yawe amesema kama mwananchi wa kawaida ana majukumu mengine ya kufanya ikiwemo kushughulikia familia yake na kuendelea kusukuma muziki wake licha ya kuwa Bobi Wine ni mdogo wake
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Neteze” amesema amechoshwa kutatua ugomvi wa bobi wine na wasanii wenzake hivyo atasusia kupokea lalama kutoka baadhi ya wasanii ikizingatiwa kuwa ni watu wazima.
Hata hivyo amehapa kumaliza ugomvi ulioibuka kati ya Bobi Wine na Eddy Kenzo kabla kuacha kabisa masuala ya kuwa mtatuzi wa mdogo wake bobi wine na wasanii wenzake.