
Mwanamuziki wa Marekani wa miondoko ya R&B, R Kelly amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na mabinti wadogo.
R. Kelly, amepatikana na hatia ya kulazimisha, kushawishi na usafirishaji wa kingono wa binti aliyekuwa chini ya miaka 18.
Tuhuma za uhalifu wa kingono zinazomkabili R. Kelly zilijulikana kwa umma baada ya vuguvugu la Me Too kuanza mnamo mwaka wa 2017.
Utakumbuka R. Kelly alikamatwa Februari mwaka wa 2019 kwa madai ya unyanyasaji wa kingono uliokithiri