Entertainment

ABIGAIL CHAMS AWEKA WAZI MATAMANIO YA KUPATA TUZO YA GRAMMY.

ABIGAIL CHAMS AWEKA WAZI  MATAMANIO YA KUPATA TUZO YA GRAMMY.

Msanii nyota wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Abigail Chams amesema lengo lake kubwa ni kushinda tuzo ya Grammy miaka michache ijayo.

Abigail ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake “U & I” amesema ni furaha kwake kujiunga na familia ya Sony Music Africa na anaamini kupitia wao atafanikisha lengo lake kwani ni lebo kubwa duniani.

“Kiukweli najisikia vizuri kuweza kuipata hiyo fursa kusainiwa na lebo kubwa duniani, Sony Music. Malengo yangu ni kupeleka Bongofleva, muziki wa Kitanzania kimataifa zaidi, na sasa hivi natazama tuzo za Grammy, nawaza kuzipata kwa miaka miwili ijayo, kwa sababu ziko hapo kwenye malengo na nina amini nitazipata lakini naamini hata BET nitazipata,” amesema Abigail Chams kwenye mahojiano na Lil Ommy.

Ikumbukwe, Abigail Chams ni msanii wa pili wa Bongofleva kusainiwa na Sony Music Africa kwa mwaka huu baada ya Young Lunya. Aidha, tayari wote wawili wameachia nyimbo zao mpya, U&I na Vitu Vingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *