Entertainment

BURNA BOY AWEKA REKODI KUPITIA ALBUM YAKE MPYA LOVE DAMINI

BURNA BOY AWEKA REKODI KUPITIA ALBUM YAKE MPYA LOVE DAMINI

Mwanamuziki kutoka Nigeria Burna Boy ameachia rasmi album yake mpya “Love Damini” yenye jumla ya ngoma 19 ikiwa na kolabo 9 pekee, huku kubwa nikutoka kwa wasanii wa Kimataifa akiwemo Ed Sheeran, J Balvin na Khalid.

Good news, Album mpya ya Burna Boy “Love, Damini” imekuwa Album ya Kiafrika iliyoshika nafasi za juu zaidi kwenye chart za US iTunes baada ya kukamata namba 2 ikiwa ni chini ya masaa machache tangu iachiwe rasmi leo Julai 8.

“Love Damini” ni album ya sita kwa Burna Boy baada ya kupata mafanikio makubwa na album yake ‘Twice as Tall’ iliyotoka mwishoni mwa mwaka 2020.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *