
Staa wa muziki nchini Mejja amefunguka kuhusu suala la mpenzi wake wa zamani Milly Wairimu kuzungumzia vibaya kwenye mitandao ya kijamii.
Kupitia mahojiano na Nicholas Kioko amesema hana muda wa kupishana na ex wake huyo kwa kuwa ana mambo mengi muhimu anayojishughulisha nayo.
Kuhusu ishu ya kubeba tumbler kwenye nyimbo zake, Mejja amesema alipata wazo la kubeba tumbler hiyo baada ya kugundua kuwa kuna mchekeshaji mmoja kwenye mitandao ya kijamii alikuwa anatumia video zake akiwa amebeba tumbler kwenye video zake za ucheshi.
Hitmaker huyo wa “Kanairo Dating” ametangaza mpango wa kugeuza tumbler kuwa biashara kwani amekuwa na mpango wa kuanza kuzalisha na kuuza tumbler kwa bei nafuu kwa wakenya.
Mbali na hayo Mejja ameamua kumpa Clemmo maua yake akiwa hai kwa kusema kuwa mhasisi huyo wa Carlif Records ndiye alimkingia kifua kipindi anaanza muziki yaani alimpa malazi, chakula na kumsaidia kimuziki na ndio maana huwa anamtaja sana kwenye nyimbo zake.
Pia ametupasha mapya kuhusu maendeleo ya album yake mpya kwa kusema kuwa ilipaswa kutoka kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti ila kuna mambo hayakuenda sawa, hivyo amewataka mashabiki wakae mkao wa kula kupokea album hiyo ndani ya mwaka huu.
Hata hivyo amewataka vijana kujiepusha na viongozi wanaoeneza siasa za chuki na migawanyiko na badala yake wawe mstari wa mbele kuhubiri amani na mshikamano wakati huu taifa linapoelekea kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.