
Staa wa muziki nchini Marekani Justin Bieber anayo furaha kukutangazia kwamba amerejea tena stejini ambapo ziara yake “Justice World Tour” imetajwa kuwa itaendelea tena Julai 31 mwaka huu nchini Italia.
Hii inakuwa taarifa njema kwa mashabiki wa Justin Bieber ambao walipigwa na ganzi baada ya tamko la kuahirishwa kwa ziara hiyo mwezi uliopita kufuatia tatizo la Kiafya lililomkumba ambapo alituweka wazi kuwa amepooza kwa muda upande wa kulia wa uso wake.