
Hit Maker wa Nakupenda, msanii Jay Melody amefunguka juu ya hisia zake kwa Paula Kajala.
Hii imekuja baada ya kumpost Mrembo huyo kwenye Ukurasa wake wa Instagram na Kuifuta baada ya Muda.
Akiwa kwenye kipindi cha Refresh cha Wasafi TV ametolea ufafanuzi mpaka kupost picha ya Mrembo huyo na baAdae kuifuta hakuwa na nia mbaya kwa Paula kwani alikuwa anamuonyesha upendo wa kawaida.
“Mimi therealpaulahkajala Nampenda kama watu wengine ninavyowapenda naziona picha zake nzuri ndio maana nikaamua kumpost lakini nilichokiandika havihusiani na picha yake ndio maana nilitanguliza picha yangu. Hakuna ubaya katika hilo.
“Hakuna mtu yoyote alienicheki lakini picha niliifuta baada ya kuona Coment zimekuwa Nyingi hadi wajomba zake nikaona sina haja ya kumtengenezea mtoto wa watu Mawazo nikaona ni bora niifute” Amesema Jay Melody.