
Mrembo Zari The Bosslady amezidi kuandamwa na page fake kwenye mitandao ya kijamii zinatumia jina lake na kuwalaghai watu wanatoa misaada kumbe lengo ni kuwaibia.
Zari alishawahi kushtakiwa kutokana na utapeli uliofanyika kupitia page fake ya Facebook iliyotumia jina lake, hivyo kuwataka kushabiki wake kuwa makini.
Kwa sasa amewaomba mashabiki wake ku-report channel ya YouTube inayotumia jina lake kwani tayari amefikishiwaa malalamiko kuhusu utapeli unaofanywa kupitia channel hiyo.
Zari kutokea Uganda anayeishi Afrika Kusini na watoto wake watano, ni miongoni mwa wanawawe wenye nguvu kubwa ushawishi kwenye mitandao, hivyo baadhi ya watu kutumia hiyo kama fursa kujifunuisha kinyume cha sheria.