Entertainment

SHEEBAH KARUNGI KUZINDUA CHUO CHA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE.

SHEEBAH KARUNGI KUZINDUA CHUO CHA KUHAMASISHA WATOTO WA KIKE.

Mwanamuziki wa lebo ya muziki ya Team No Sleep Sheebah Samali Karungi amefunguka na kusema kwamba ana mpango wa kuanzisha shule ya kutoa ujuzi wa kuwahamasisha watoto wa kike.

Hitmaker huyo wa Yolo amesema lengo la yeye kuanzisha chuo hicho ni kuwaona wanawake wanaanza kujitegemea kiuchumi badala ya kukaa nyumbani wakisubiri waume zao wawape pesa na mahitaji ya msingi.

Sheebah amedokeza kwamba ataendelea na mpango wake wa kutoa msaada kwa jamii maeneo yote nchini uganda kwa lengo la kuwahimiza watoto wa kike wajenge tabia ya kujitegemea katika maisha.

Kauli ya Sheebah imekuja mara baada ya kuulizwa kama ana mpango wa kuanzisha chuo cha muziki ambacho kitakuza vipaji nchini uganda ili itoe  wasanii wenye tajriba kama yake

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *