
Rapa Fetty Wap amekiri kuwa na hatia ya kutekeleza kosa la kumiliki na kusambaza Gram 500 za dawa za kulevya aina ya Cocaine. Kosa hilo linabeba hukumu ya chini ya miaka 5 Jela.
Oktoba mwaka 2019, Rapa huyo alikamatwa na FBI akiwa na wenzake sita kwenye tamasha la Rolling Loud ambapo wote walifunguliwa mashtaka ya kumiliki na kusambaza dawa za kulevya.
Tarehe ya hukumu yake haijatajwa hivyo Willie Junior Maxwell maarufu Fetty Wap ataendelea kubaki rumande kutokana na dhamana yake kubatilishwa