Entertainment

MBOGI GENJE WAWEKA WAZI SABABU ZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA

MBOGI GENJE WAWEKA WAZI SABABU ZA KUMUUNGA MKONO RAILA ODINGA

Kundi la Mbogi Genje limefunguka sababu za kumuunga mkono kiongozi wa mrengo wa kisiasa wa Azimio la Umoja kwenye uchaguzi wa Agosti 9 mwaka huu.

Katika mahojiano yao na 2mbili wasaniii wa kundi hilo wamesema walitoa wimbo kwa ajili ya kumsifia Raila Odinga kwa sababu walifuata upepo wa kisiasa nchini ambao ulikuwa unazungumzia sana kiongozi huyo wa kisiasa.

Aidha wamepongeza hatua ya Raila Odinga kuelekea mahakamani kupinga matokeo ya urais kwenye uchaguzi uliokamilika kwa kusema kwamba alifanya jambo la busara badala ya kuwachochea wafuasi wake kuzua vurugu.

Kitu kingine ambacho Mbogi Genje wamekizungumzia ni kuhusu ishu ya kumtenga member mwenzao Guzman kwa kusema kwamba ameshikika kwenye majukumu mengine, hivyo hawajamtoa kwenye kundi lao kama jinsi watu wanavyozungumza mitandaoni.

Utakumbuka Mbogi genje ni kundi la linaloundwa na wasanii watatu ambao ni Militan, Guzman na Smady.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *