
Staa wa muziki kutoka Marekani Lil Baby ameshinda takriban shillingi millioni 120 za Kenya kwenye mchezo wa bahati nasibu maarufu Casino.
Baada ya kushinda mkwanja huo, Lil Baby amewabariki washkaji zake kwa kuwapa shillingi millioni 1.2 kila mmoja.
Kupitia Twitter Lil Baby ameachia ujumbe usemao “Wanajua nimeshinda pesa, lakini wasichokijua ni kwamba sipo hapa kula bata, ninawekeza.”
Kwa wasiofahamu, Lil Baby alikuwa mcheza kamari mzuri tu kabla ya kuingia kwenye muziki.