Entertainment

OTILE BROWN AZUA GUMZO MTANDAONI NA SOKSI YA KSHS. 32,000

OTILE BROWN AZUA GUMZO MTANDAONI NA SOKSI YA KSHS. 32,000

Msanii nyota nchini Otile Brown ameamua kuzitumia ipasavyo pesa anazozikeshea na kuzitolea jasho.

Mkali huyo wa “Celebration” kupitia Instastory ametuonesha soksi ambazo kwa mujibu wake zilimgharimu shillingi 32,000 za Kenya.

Hatua hiyo imeonekana kuleta ukakasi miongoni mwa mashabiki zake, wengi wakionekana kumkejeli kwa kusema kuwa anatumia suala hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni

Hii sio mara ya kwanza kwa Otile Brown kuanika vitu vya thamani anavyovimiliki, mapema mwaka huu alitusanua kuwa alitumia kiasi cha shillingi elfu 80 za Kenya kununua viatu aina Balenciaga Crocs boots.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *