Entertainment

EXRAY KUTUMBUIZA KWENYE HHAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WILLIAM RUTO

EXRAY KUTUMBUIZA KWENYE HHAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WILLIAM RUTO

Msanii Exray Taniua ametajwa kutumbuiza kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais mteule William Ruto Jumanne juma lijalo.

Mapema wiki hii hitmaker huyo wa “Sipangwingwi” aliposti video akiwa anakutana na rais huyo mteule na kisha kumpongeza kwa kuhifadhi ushindi wake baada ya mahakama ya juu kutupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya urais iliyowasilishwa na Azimio la Umoja.

Exray atakuwa kwenye jukwaa moja na Guardian Angel, Solomon Mkubwa na wasanii wengine wengi ambao watatoa burudani kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais William Ruto ambayo itahudhuriwa na marais wa mataifa mbali mbali.

Guardian Angel na mke wake Esther Musila wameposti pia video wakiwa kwenye matayarisho katika uga wa Kimataifa wa Kasarani ambako hafla hiyo itafanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *