
Rapa kutoka Marekani PNB Rock ameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo kwenye tukio la uvamizi lililotokea kwenye mgahawa mmoja Jijini Los Angeles.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Jijini Los Angeles, Kelly Muniz, rapa PNB Rock mwenye umri wa miaka 30 alikuwa na mpenzi wake kwenye mgahawa huo, ambaye aliweka location kwenye picha ambayo tayari imefutwa Instagram.
Inaelezwa kwamba mtu mmoja ambaye bado hajafahamika alivamia mgahawa huo akiwa na silaha na kutaka vitu kutoka kwa marehemu PNB Rock ikiwemo vito vya thamani. Lakini dakika chache baadaye mtu huyo aliishia kufyatua risasi na kumpiga rapa huyo ambaye alikimbizwa hospitali na kufariki baada tu ya kufikishwa.
PNB Rock ambaye alizaliwa mwaka 1991 alitapata umaarufu kwenye muziki wa Hiphop duniani kupitia wimbo wake uitwao “Selfish” ambao ulikamata nafasi ya 51 kwenye chati ya US Billboard Hot 100.
Katika kipindi cha uhai wake alifanikiwa kuachia album 2 za muziki, mixtape 5, EP moja na singo 19.