
Mke wa msanii John Legend, Chrissy Teigen amefunguka kuhusu tukio la huzuni ambalo lilimtokea miaka miwili iliyopita ambapo alimpoteza mtoto wake ambaye hakuwa amezaliwa.
Kwenye mahojiano yake mapya, Teigen mwenye umri wa miaka 36 amesema alimpoteza mtoto huyo kutokana na kutolewa kwa ujauzito (abortion) na sio kuharibika kwa mimba (miscarriage) kama ambavyo ilielezwa.
Teigen amesema alishtuka kugundua kwamba alifanyiwa ‘abortion’ ili kunusuru maisha yake kwa mtoto ambaye hakuwa na nafasi tena ya kuishi.
Mwanamama huyo amesema ilibidi asizungumze ukweli kutokana na jamii kuona kitendo hicho ni cha ajabu na kisichokubalika, hivyo ikabidi adanganye kwa kusema ujauzito ule uliharibika (miscarriage).
Utakumbuka Chrissy Teigen ambaye kwa sasa ni mja mzito amejaliwa kuwapata watoto wawili pamoja na John Legend.