
Hitmaker wa “Utu”, Msanii Ali Kiba ametangaza kurejea kwa ziara yake ya muziki nchini Marekani “Only One King” ambayo alitangaza kuiahirisha Septemba 1, mwaka 2022 kufuatia kugundulika kuwa na ugonjwa wa Corona.
Ziara hiyo ambayo ilikuwa ianze September 2, sasa imetangazwa kurejea kuanzia mwezi Oktoba na Novemba mwaka huu. Aidha King Kiba amesema tarehe rasmi zitatangazwa hivi karibuni.
“My USA Fans, After A Little Delay Due to Reasons Beyond Our Control, I’m Happy To Announce “My Only One King US Tour” is Back This October-November. New Dates and Cities To Be Announced Soon. For Bookings & Inquiries Please Call 323.868.6114” Ameandika Instagram.
Only One King US Tour 2022 inatarajiwa kufanyika Houston, Minneapolis, Phoenix, Des Moines, Atalanta, Lexington, Manchester, Chicago na Dallas.