Entertainment

SHEEBAH KARUNGI MBIONI KUHALALISHA NDOA YAKE KWA NJIA YA HARUSI

SHEEBAH KARUNGI MBIONI KUHALALISHA NDOA YAKE KWA NJIA YA HARUSI

Msaniii kutoka Uganda Sheebah Karungi ametangaza kuhalalisha mahusiano yake kwa kufanya harusi mwezi Disemba mwaka huu kutokana na watu wengi kumshinikiza kuingia kwenye ndoa miaka ya hivi karibuni.

Kupitia video aliyo-share kwenye mitandao ya kijamii Hitmaker huyo a “Kansalewo” amesema kuwa hafla ya harusi yake itafanyika Disemba 9 katika hoteli ya Serena Jijini Kampala sambamba na tamasha lake la muziki.

Hata hivyo walimwengu wametilia shaka kauli ya Sheebah Karungi kwa kusema kuwa huenda mrembo huyo anatengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni kwa ajili ya kutangaza tamasha lake la muziki.

Sheebah Karungi ambaye kipindi cha nyuma alidai kuwa haamini kwenye masuala ya ndoa alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na meneja wake wa zamani Jeff Kiwa lakini uhusiano wao ulikatishwa na jini mkata kamba baada ya meneja wake huyo kumsaliti kimapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *