
Rapa wa kike nchini Noti flow amefunguka kuhusu tatizo la kiafya ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda sasa.
Kupitia mfululizo wa instastory yake kwenye mtandao wa Instagram mrembo huyo amekiri kuwa amekuwa akipata shida sana kwenye suala la kula chakula, jambo ambalo limemuathiri kiafya kiasi cha kupungua kimwili.
Noti Flow amesema licha ya kupata maelekezo kutoka kwa daktari ya namna ya kukabilia na tatizo hilo, alishindwa kufuata taratibu alizopewa na mhudumu wake wa afya kutokana na yeye kukosa hamu ya kula.
Hata hivyo ameahidi kufanya kila awezalo kuhakikisha anashirikiana kwa ukaribu na daktari kwa ajili ya kuuweka mwili wake sawa.