
Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametoa angalizo kwa watoto wa kike kuwa wangalifu kabla ya kuchukua maamuzi ya kupata uja uzito.
Nadia amesema wanawake kwa asilimia kubwa ndio hubeba majukumu ya kumlea mtoto ikilinganishwa na wanaume, hivyo wanapaswa kujipanga kisaikolojia kukabiliana na changamoto za kuwa mzazi ikiwemo mabadiliko ya kimwili na kimuonekano.
Katika hatua nyingine Nadia Mukami amesema kuwa kutokana na changamoto zinazowakumba akina mama wachanga kwenye masuala ya malezi ana mpango wa kushirikiana na mume wake Arrow Boy kuja na podcast ambayo itakuwa mahsusi kwa ajili ya kuhamasisha vijana kuhusu athari za mimba ya utotoni.