
Baada ya kutumbuiza kwenye michuano ya Kikapu maarufu kama Basketball Africa nchini Rwanda wiki moja iliyopita, kundi la sauti sol limetajwa kama wasanii vinara kwenye uzinduzi wa tamasha la Afropalooza oktoba 9 mwaka huu nchini uganda.
Wasanii wengine watakaowasha moto wa burudani siku hiyo ni pamoja na, Cindy, Lilian Mbabazi, Spice Diana, Maurice Kirya, Ykee Benda, Winnie Nwagi, Vinka, Navio.
Tamasha la Afropalooza ambalo litafanyika kati ya tarehe 7 na 9 Oktoba katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval, jijini Kampala litawaleta pamoja zaidi ya wasanii 60.