
Bosi wa Konde Music Worldwide, Msanii Harmonize ameendelea kutoa ya moyoni baada ya aliyekuwa mke wake, Sarah kwenda Mahakamani.
Katika mazungumzo na mchumba wake wa sasa Kajala Masanja, amesema sababu ya Sarah kudai talaka ni kuwa anataka wagawane mali.
Msanii huyo amedai kuwa hakuna mali yoyote ambayo anapaswa kugawana na mwanamitindo huyo kutoka Italia huku akibainisha kuwa aliondoka bila chochote wakati walipoachana mwishoni mwa mwaka 2020.
Hata hivyo Harmonize anapanga kuandika talaka tatu baada ya ex-wake huyo kuwasilisha kesi mahakamani kudai talaka yake.
Utakumbuka Harmonize na Sarah walifunga ndoa Septemba mwaka 2019 na waliachana Desemba mwaka 2020 ukiwa ni mwaka mmoja tu wa ndoa yao.