Entertainment

Mwanamuziki Ronald Alimpa aomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki Ronald Alimpa aomba msaada wa kifedha kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki kutoka Uganda Ronald Alimpa anaomba msaada wa kifedha baada ya kuhusika kwenye ajali mbaya ya barabarani Septemba 29 mwaka huu.

Kwenye video inayosambaa mtandaoni alimpa ambaye amelazwa hospitalini amewaomba mashabiki, wanafamilia, marafiki na wahisani kumchangishia pesa ili aweze kulipa gharama ya matibabu.

Ronald Alimpa na msanii Lady Grace na Ragga Fire walihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani huko Ssemuto Katika wiliya ya Nasakeseke jana Alhamisi.

Lakini kwa bahati mbaya  msanii lady grace alifariki dunia papo hapo huku akiwaacha wengine na majeraha mabaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *