Entertainment

Harmonize azima tetesi za lebo ya Konde Gang kufilisika

Harmonize azima tetesi za lebo ya Konde Gang kufilisika

Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Harmonize amewafunga mdomo wale wote waliodhani kuwa ameshindwa kuendesha lebo ya Konde Gang.

Kupitia insta stori yake kwenye mtandao wa Instagram amefichua mpango wa kutambulisha makao mapya ya lebo hiyo sambamba na kuwasajili wasanii wapya Oktoba 10 mwaka huu wakati Konde Gang itaandhimisha miaka mitatu tangu kuzinduliwa kwake.

Hitmaker huyo wa “Leave Me Alone” amewashukuru mashabiki kwa kusimama na lebo ya Konde Gang huku akisisitiza kuwa lebo hiyo itaendelea kukuza vipaji vya vijana wasiojiweza kwenye jamii.

Kauli ya Harmonize imekuja mara baada ya picha kusambaa kuwa Makao Makuu ya lebo ya Konde Gang yanapigwa mnada na pia kuna wasanii wanaondoka kwenye lebo hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *