
Mwanamuziki wa Bongofleva, Zuchu ametangaza kuja na bidhaa zake za mavazI
Kupitia ukurasa wa Twitter mkali huyo wa ngoma ya “Sukari” anasema kuwa kuna mitindo mipya ameianzisha yeye kama viatu vya midoli,kusuka rasta ndefu pamoja na kuvaa nguo kubwa vyote siku hizi watu wanafanya kwa sababu yake.
“Vile Naskia raha nikiona watu wanavaa teddy bear, slippers (viatu vya mdoli) nikiona tu najipa bonge la tano kwamba yeah you did that Zuuh.
“Coming with my own brand soon na nitalenga asilimia kubwa ya Watanzania wenzangu tutapendeza kwa bajeti.” Ameandika Zuchu