
Ni miezi mitano sasa imepita tangu Rihanna ajifungue mtoto wa Kiume, lakini hadi leo hajaanika wazi Jina la mtoto wala uso wake kwenye mitandao ya kijamii. Mashabiki zake wameanza kujiongeza na kulitafuta Jina la mtoto huyo hata kupitia mavazi ambayo anavaa Riri kwenye mitoko.
Wikendi hii Riri alionekana akiwa amevaa cheni ndefu yenye herufi ‘D’ hivyo kuwafanya mashabiki zake wa nguvu kuhisi labda Jina la mtoto huyo linaanza na herufi hiyo. Kuna wengine ambao waliwahi kujiongeza na kudai Jina litakuwa linaanza na herufi ‘R’ kutokana na majina halisi ya Rihanna (Robyn) na A$AP Rocky (Rakim)