
Mwanamuziki wa Bongofleva Whozu ameashiria kufunga pingu za maisha na mwigizaji Wema Sepetu mwaka 2023.
Whozu alidokeza hayo kwa kuacha comment kwenye Instagram kupitia ukurasa wa Sepetu na kumwita mke wake kisha kuweka ishara ya Pete ya ndoa na emoji ya Bibi harusi.
Whozu ameandika; “2023 …. Wifey
” ikiwa ni kiashirio kwamba uhusiano wao kuvuka kwenda hatua nyingine kubwa.
Wawili hao ambao mahusiano yao kwa mara ya kwanza waliyaweza wazi kwa mashabiki wao kwenye siku ya kumbukizi ya kuzaliwa ya Wema Sepetu, Septemba 28.