
Rapa Majirani amefunguka sababu kuacha kazi ya ujenzi aliyokuwa anafanya nchini Qatar na Saudia Arabia.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema aliamua kurejeni nchini kwa ajili ya matatizo ya kifya yaliyotokana na kuzidiwa athari ya viwango vya juu vya joto katika nchini za miliki ya kiarabu
Hitmaker huyo wa “Tukumbukeko” amesema kwa sasa ana mpango wa kurejea shuleni kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu, kuanzisha biashara na kukuza vipaji vya vijana mtaani kwao kupitia mchezo wa soka.
Lakini pia amedokeza ujio wake mpya kimuziki kwa kuwataka mashabiki kukaa mkao wa kula kumpokea mwakani kwani anarudia kwa kishindo na muziki mzuri kwa lengo la kuirejesha jina lake kwenye ramani ya muziki kama alivyokuwa anafanya kipindi yupo nchini ya lebo ya muziki ya Grand pa Records.
Hata hivyo Majirani amemamilizia kwa kuwataka wasanii waache kujificha kwenye maisha ya ustaa na badala yake wafanya shughuli zitakazowaingizia kipato kwa kuwa muziki haulipi kutokana na ukosefu mazingira mazuri ya kuwasaidia vijana kujiajiri kupitia muziki wao.