
Waandaji wa tuzo za Muziki nchini Marekani maarufu kama (American Music Awards) wametoa orodha ya wasaniii watakaowania tuzo hizo mwaka huu ambapo Beyonce na Taylor Swift wameongoza kwa kutajwa zaidi kwenye vipengele wakiwa wametajwa mara 6 kila mmoja.
Gumzo limekuja baada ya kuonekana kipengele maalum cha Muziki wa Afrobeats kwenye Tuzo hizo ambacho kinaitwa (Favorite Afrobeats Artist) na kimewakutanisha wasanii wa Nigeria pekee akiwemo Burna Boy, CKay, Wizkid, Tems na Fireboy DML.
Katika hatua nyingine Tems ametajwa pia kwenye kipengele cha Kolabo Bora ya mwaka kupitia ngoma ambayo ameshirikishwa na Future pamoja na Drake “Wait For U” lakini pia wimbo wa Wizkid na Tems “Essence” umetajwa kwenye kipengele cha Favorite R&B Song