
Staa wa muziki kutoka Marekani Tory Lanez ametoa angalizo kwa wanaume wawe makini na wadada wa karne hii kwa kuwa ni waongo kupitiliza.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Tory Lanez amewataka wanaume kutowaamini wasichana haswa kwenye masuala ya mapenzi.
“Baadhi ya wasichana wanaweza kukufanya uhisi kwamba wanaweza kujiua kama utaachana nao. Niko hapa kuwaambia washkaji zangu Mwanamke hawezi kujitoa uhai, Hiyo hali itamuondoka tu Jiokoe mwenyewe”, Ameandika.
Hata hivyo hajajulikana ni kitu gani kimemfanya rapa huyo kutoa kauli hiyo yenye ukakasi ila walimwengu wamehoji huenda kuna mwanamke amepiga tukio la mwaka kwenye mahusiano yake kiasi cha kumuacha na makasiriko ya kuvunjwa moyo.