Entertainment

Megan Thee Stallion avamiwa, wezi waondoka na mali ya mamilioni

Megan Thee Stallion avamiwa, wezi waondoka na mali ya mamilioni

Nyumba ya Rapa Megan Thee Stallion ya mjini Los Angeles, nchini Marekani imevamiwa na majambazi ambao walifanikiwa kuiba vitu vyenye thamani ya takribani shillingi millioni 36 za Kenya.

Tovuti ya TMZ imeripoti kwamba watu wawili walionekana wakivunja milango na kuingia kwenye nyumba hiyo hadi chumbani ambapo waliiba vito vyake vya thamani na pesa taslimu.

Wakati tukio hilo linatokea, Megan Thee Stallion hakuwepo ndani, alikuwa mjini New York ambapo baada ya kupata taarifa hizo aliingia Twitter na kuelezea hisia zake lakini pia kutangaza kuchukua mapumziko kwenye muziki baada ya onesho lake kwenye kipindi cha Saturday Night Live (SNL) wikendi hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *