Entertainment

David Lutaalo amtaka Gravity Omuttuju kuomba kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe

David Lutaalo amtaka Gravity Omuttuju kuomba kwa kuwavunjia heshima wasanii wakongwe

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda David Lutaalo amemtaka rapper Gravity Omutujju kuwaomba msamaha wasanii Jose Chameleone, Bobi Wine na Bebe Cool kwa matamashi ya chuki dhidi yao.

Kwenye mahojiano yake hivi karibuni, Lutaalo amesema hatua ya rapa huyo kujilinganisha kisanaa na watatu hao ni kuivunjia heshima tasnia nzima ya muziki nchini uganda ikizingatiwa kuwa hajafanikiwa hata kupata nusu ya mali ambayo wasanii hao wameingiza kupitia muziki wao.

Mapema mwezi huu Gravity Omutujju aliibuka na kujinasibu kuwa yeye ndio  mwanamuziki bora zaidi kuwahi kutoka nchini uganda kuwazidi Jose Chameleone, Bobi Wine na Bebe Cool ambapo alieda mbali zaidi na kuwataka watatu hao kustaafu muziki kwa ili kutoa nafasi kwa wasanii wapya kung’aa kisanaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *