Sports news

ARSENE WENGER ASEMA KUNA UWEZEKANO WA OFFSIDE KUAMULIWA NA TEKNOLOJIA MWAKA 2022

ARSENE WENGER ASEMA KUNA UWEZEKANO WA OFFSIDE KUAMULIWA NA TEKNOLOJIA MWAKA 2022

Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba maamuzi ya ‘Offside’ yakaamuliwa moja kwa moja kwa kutumia Teknolojia kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyika nchini Qatar.

Wenger ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa maendeleo ya mpira wa miguu katika Shirikisho la Soka duniani FIFA, amesema hiyo itakuwa hatua kubwa kwenye soka la dunia kwani pia itapunguza lawana nyingi kwa waamuzi. Kwa sasa teknolojia imechukua nafasi kubwa kwenye mpira kwani maaumizi mengi nyeti yanafanywa na VAR na Goal Line Technology.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *