
Kundi la muziki maarufu kutoka nchini Tanzania Navy Kenzo wametajwa kuwa ni moja wapo ya wasanii watakao unda tracklist ya album iliyoandaliwa na Kampuni ya usambazaji wa muziki ya EMPIRE iliyopo San Francisco, Marekani.
Taarifa hiyo ambayo imethibitishwa na ukurasa rasmi wa instagram wa Empire Africa pia ikiandikwa kwenye tovuti kubwa kama Billboard, Hot97 na Variety za nchini marekani, album hiyo inatajwa kuwa na mjumuisho wa mastaa wa muziki kutoka Afrika wakiwemo Olamide, Fireboy DML, Kizz Daniel, Buju BNXN, Asake, Black Sherif na wengineo wengi.
Album hiyo imepewa jina la “Where we come from” na inatarajiwa kutoka mwezi ujao, Novemba 18, 2022.
Utakumbuka Empire Africa wameamua kuja na album hii baada ya muziki kutoka barani Afrika kusikilizwa na kupendwa kwa kiwango kikubwa Duniani.