Entertainment

Trio Mio atoa ujumbe muhimu kwa familia na mashabiki katika siku yake ya kuzaliwa leo.

Trio Mio atoa ujumbe muhimu kwa familia na mashabiki katika siku yake ya kuzaliwa leo.

Rapa anayekuja kwa kasi nchini Trio Mio ameshindwa kuficha furaha yake baada ya kufikisha umri miaka 18, Oktoba 22.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika ujumbe mzito wa shukrani kwa familia, mashabiki na uongozi wake kwa kusimama naye kwenye safari yake ya muziki.

“I’m officially legal! Just turned 18 today fam na naskia wah! Tuzidi kuzidi in this journey together. I thank God, my mama for giving birth to this fine pikin my sisters for always being there for me, my bro for being my shield, my team for the amazing work we do and you my fans for sticking with me through my growth as an artist. Kijana ako 18 na namada mesti Dec, mustake jua vile nakam na ubaya”, Ameandika.

Hitmaker huyo wa “Cheza Kama Wewe” amesema zawadi kubwa ambayo mashabiki zake wanaweza kumpa kwenye kumbukizi ya kuzaliwa kwake ni kuitazama video ya wimbo wake mpya uitwao “Hapa Kazi Tu.” inayopatikana kwenye mtandao wa Youtube.

“Biggest gift mnaeza nipea ni kucheki ngoma yangu mbichi #HapaKaziTu. Like, comment, share & subscribe. Link kwa bio “, Ameongeza.

Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali nchini akiwemo Nameless na Bien wa Sauti Sol wametakia msanii huyo salamu za heri kipindi hiki anasherekea kumbukizi ya kuzaliwa kwake.

Utakumbuka Trio Mio kwa sasa anajianda kukalia mtihani wake wa kidato cha nne na juzi kati alitoa angalizo kwa wasanii wajipange kimuziki kwani atakaporejea kwenye tasnia ya muziki atawaonyesha kivumbi kwa kuachia nyimbo kali mfululizo bila kupoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *