Entertainment

Harmonize atangaza utaratibu mpya wa Promotion ya Album yake mpya.

Harmonize atangaza utaratibu mpya wa Promotion ya Album yake mpya.

Staa wa muziki nchini Harmonize ametangaza rasmi hatoifanyia promotion album mpya kama ilivyoozeka kwa wasanii wengine kufanya mkutano na waandishi wa habari, Ziara kwenye vyombo vya habari, kuweka bango lolote barabarani au kufanya listening party.

Harmonize amebainisha hayo kupitia insta story yake kwa kueleza kwamba ameshafanya kila kitu (studio), hivyo anataka mashabiki wasikilize muziki mzuri aliouandaa. Na pia ameongeza, ikiwezekana ataishare mara moja tu kwenye platform zake.

Kauli ya Harmonize imekuja mara baada ya kutangaza kuachia Album yake ya tatu itwayo Made For Us Oktoba 28 mwaka huu na tayari ametuonesha Tracklist yenye Jumla ya nyimbo 14.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *