
Mwimbaji wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya Dazlah hatimaye ameachia rasmi Extended Playlist (EP) mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.
Dazlah amewabariki mashabiki zake na EP iitwayo The Future yenye jumla ya ngoma 5 za moto ambapo ngoma zote amehusu mwenyewe.
Ngoma zinazopatikana kwenye EP hiyo ni pamoja na “Naogopa”, “Tamaa”, “Waru Waru”, “Baisho” na “Pisi Kali”
The Future ambayo ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Dazlah katika safari yake ya muziki, tayari inapatikana kwenye majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mitandaoni (Digital Platforms).
Ikumbukwe Dazlah kwa sasa yupo chini ya uongozi wa Shirko Media mara baada ya kusaini mkataba wa kudumu na kampuni hiyo kusimamia shughuli zake za muziki.