Entertainment

Ommy Dimpoz anyosha maelezo juu ya kuwashirikisha wasanii wa kifaransa kwenye album yake mpya

Ommy Dimpoz anyosha maelezo juu ya kuwashirikisha wasanii wa kifaransa kwenye album yake mpya

Msanii wa Bongofleva, Ommy Dimpoz amesema wamewashirisha Fally Ipupa kutokea DR Congo na DJ Kerozen wa Ivory coast katika albamu yake ili kupata wasikilizaji wengi kwenye nchi zinazozungumza Kifaransa.

Albamu hiyo inayokwenda kwa jina la Dedication ilitoka Ijumaa hii ikiwa na nyimbo 10, hii imesimamiwa na Rockstar Africa na Sony Music Africa.

Wasanii wa Bongofleva walioshirikishwa katika albamu hiyo ni Nandy na Marioo.

Ommy Dimpoz amesema DJ Kerozen ni msanii maarufu sana Afrika Magharibi wanapozunguza sana Kifaransa, hivyo anaamini hiyo itaibeba vilivyo albamu yake, hivyo hivyo upande wa Fally Ipupa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *