
Album ya mwimbaji kutoka Konde Gang, Ibraah “The King Of New School” iliyotoka Julai 1, mwaka huu, ikiwa pia ndio album yake ya kwanza katika safari yake ya muziki, imefanikiwa kufikisha jumla ya streams Milioni 12 katika majukwaa yote inapopatikana album hiyo.
Hii ni habari njema kwa mashabiki wa msanii Ibraah kwani album hiyo imetumia miezi mitano pekee kupata namba hiyo kubwa. “The King Of New School” yenye jumla ya ngoma 17, Ibraah amewakutanisha wakali kama Christian Bella, Bracket, L.A.X na wengine wengi toka Afrika.
Aidha, Ibraah ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru mashabiki wake kwa album yake kufikisha jumla ya streams Milioni 12.