Ibraah Ataka Usaidizi wa Masheikh Baada ya Kuachwa na Mke Wake
Msanii wa muziki wa Bongo Flava Ibraah ameshindwa kuficha maumivu yake baada ya kudai kuachwa na mwanamke aliyekuwa akimtambua kama mke wake. Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Ibraah amesema kuwa anapitia kipindi kigumu kihisia, hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ameeleza kuwa anahofia huenda hali anayopitia ikaathiri mfungo wake. Ibraah amewaomba mashabiki wake kumsaidia kuwatag Masheikh na viongozi wa kidini ili wampe mwongozo. Msanii huyo anahoji mafundisho ya Uislamu yanavyoelekeza pale mwanamke anapoamua kumuacha mwanaume aliyekuwa akimwita mume. Wakati baadhi ya mashabiki wakimpa pole na kumshauri awe na subira katika mwezi huu mtukufu, wengine wameanza kuhoji kama mwanamke huyo alikuwa mke wa ndoa rasmi au ni mahusiano ya kawaida yaliyopewa jina la mke. Hata hivyo, kwa Ibraah, pigo hili linaonekana kuwa kubwa zaidi ya muziki, likigusa maisha yake ya kiroho na mustakabali wa furaha yake.
Read More