
Mchekeshaji Eric Omondi amekanusha madai ya kutumia suala la mchumba wake kupoteza uja uzito kutafuta kiki.
Kwenye mahojiano yake hivi karibuni madai hayo hayana ukweli wowote kwani alikuwa anajaribu kuwapa vijana wenzake changamoto ikitokea wapenzi wao wamejipata kwenye hali ya kuaharibikiwa na uja uzito.
Utakumbuka mapema wiki hii Eric Omondi alichapisha video ikimuonyesha mpenzi wake akilia kwa uchungu akiwa hospitalini baada ya uja uzito wake kuaharibika( Miscarriage).
Hata hivyo Omondi alipata ukosoaji mkubwa kutoka kwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii wakihoji kuwa mchekeshaji huyo alikosea sana kuweka video hiyo mtandaoni.