
Mwanamuziki Willy Paul amewataka wasanii wa muziki nchini Kenya kufanya kazi kwa bidii na kuacha kutegemea kiki katika kukuza muziki wao.
Kupitia Insta story yake, mwanzilishi huyo wa lebo ya Saldido amewashauri wanamuziki kupunguza kutengeneza kiki ambazo zitakuja kuwaaribia kazi zao siku za mbeleni na badala yake kuweka juhudi zaidi katika kuzalisha maudhui yenye ubora.
“Ombi langu kwa tasnia ya muziki wa Kenya. Kazi Zaidi, Kiki kidogo! Hivi karibuni mtakumbuka maneno haya,” aliandika.
Hali ya tasnia ya muziki nchini Kenya imeibua mjadala mkubwa mitandaoni katika siku za hivi karibuni huku wasanii mbalimbali wakishinikiza muziki wao upewe kipau mbele zaidi kwenye vyombo vya habari huku wengine wakilalamikia kutotendewa haki na mapromota pamoja na mashabiki.