Entertainment

Burna boy atangaza kufanya onesho katika uwanja wa London.

Burna boy atangaza kufanya onesho katika uwanja wa London.

Staa wa muziki kutoka Nigeria Burna Boy anaenda kuandika historia nyingine kwenye Muziki wake, ametangaza kuwa atafanya onesho kwenye uwanja wa (London Stadium) uliopo nchini Uingereza, Juni 3 mwaka 2023. Uwanja huo una uwezo wa kubeba watu 66,000.

Burna Boy atakuwa msanii wa kwanza toka barani Afrika kufanya onesho kama msanii Kinara (Headliner) kwenye uwanja nchini Uingereza. Mshindi huyo wa Tuzo ya Grammy, tayari anaishikilia rekodi ya kuwa msanii wa kwanza barani Afrika kufanya onesho katika ukumbi wa Madison Square Garden Jijini New York.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *