Entertainment

Daddy Owen akiri kutoshiriki tendo la ndoa kwa miaka miwili

Daddy Owen akiri kutoshiriki tendo la ndoa kwa miaka miwili

Mwimbaji wa nyimbo za Injili , Daddy Owen amefichua kuwa hajashiriki tendo la ndoa kwa miaka miwili.

Katika mahojiano yake hivi karibuni, Owen amesema kuwa hajakuwa na hamu ya kufanya mapenzi tangu alipoachana na mke wake.

“Sihitaji mwanamke, sijafanya mapenzi kwa miaka miwili, mwanamke ni wa kazi gani?” Owen alisema.

Kauli yake imekuja mara baada ya kukiri kuwa hataki mwanamke kwenye maisha yake tena ikizingatiwa kuwa wiki kadhaa ilyopita alitangaza kuwa anatafuta mke.

“Sitaki hata kupikiwa, nitakula hotelini, hata wageni wakija nyumbani kwangu tutanunua chakula, sitaki kuoa tena,” mwimbaji huyo alisema.

Alisema kuwa ameridhika na maisha yake ya sasa na hatafuti mke wa kuoa kwani ana mambo mengi ya msingi ya kufanya.

“Kwa sasa nafanya mambo mengi, sitafuti tena mke. Nitafute mke wa nini? Kama ni mtoto ninaye tayari, si bora kuwa na mtoto,” Owen alisema.

Utakumbuka Daddy Owen na mkewe Farida Wambui walitengana mwaka 2020 baada ya kuwa kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka minne.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *