
Wenyeji wa michuano ya Kombe la timu ya Taifa ya Qatar imekuwa timu ya kwanza kuondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kupokea kichapo cha 3-1 kutoka kwa Senegal kwenye mchezo wa pili wa kundi A.
Simba wa Teranga Senegal imewatoa kimasomaso Waafrika kwa kuwa timu ya kwanza ya Afrika kupata ushindi kwenye michuano hiyo ya mwaka huu na kufufua matumaini ya kufuzu hatua ya mtoano kutoka katika kundi hilo.
Qatar watakamilisha ratiba tu katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo kwa kuwavaa Uholanzi.